Mchezaji wa Klabu ya Chelsea ya Uingereza anasakwa na polisi baada ya mwanamke mmoja kudai alidhulumu kijinsia.

Tayari polisi nchini Canada wametoa waranti ya kumkamata kwa makosa hayo.

Klabu ya Chelsea imekiri kuwa inafahamu kuhusu tukio hilo dhidi ya mchezaji wake Lucas Piazon.

Mchezaji huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 21 na ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Reading anadaiwa alikutana na mwanamke mmoja kwenye ukumbi wa disco mwezi julai.

Wawili hao walijivinjari na kujiburudisha kwa vileo na kisha wakaambatana sako kwa bako na kuelekea kwa nyumba moja alikoishi mwanamke huyo mjini Toronto.

Polisi nchini Canada wanadai kuwa ,Huko ndiko mchezaji huyo aliyekuwa ameambatana na mwenzake Andrey da Silva Ventura, 22 ambaye ni mlinda lango wa Brazil wanadaiwa walishindwa kujistahimili na wakamvamia kipusa huyo aliyekuwa amelala.

”waliingia ndani ya chumba chake cha kulala na kumvamia.”

”Alipoamka waliondoka na kutoweka”. ripoti ya polisi inaelezea.

Tukio hilo linaripotiwa kuwa lilitokea siku ileile ambayo mshambuliaji huyo wa Chelsea alikuwa ameifungia Brazil bao katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Panama.

Brazil ilishinda nishani ya shaba katika mashindano hayo ya Pan-Am yaliyoandaliwa Canada mwezi Julai.

Msimu huu Piazon amefunga mabao mawili katika mechi 8 alizoichezea Reading.

Muamuzi Afungiwa Chumbani
Kocha Wa Njombe Mji Alazwa Muhimbili