Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Meddie Kagere amazima minong’ono ya wadau wa soka nchini kuhusu kuanza vibaya kwa Simba SC katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, baada ya kuifungia bao la ushindi timu hiyo kwenye mchezo wa mzunguuko wa pili mjini Dodoma.

Simba SC walikuwa na kazi kubwa ya kuikabili Dodoma Jiji FC ambayo ilikua wenyeji wa mchezo huo, na Kagere alilazimika kusubiri hadi katika dakika ya 70 kupachika bao la ushindi.

Kazi kubwa ilifanywa na Mshambuliaji Chriss Mugalu baada ya kupiga kichwa mpira uliotoka kwa Mlinda Lango Aishi Manula, na ndipo ulimkuta Meddie Kagere na kufunga bao hilo muhimu.

Ushindi huo unaipaisha Simba SC hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 4, huku ikicheza michezo miwili mpaka sasa.

ASA waanza kusambaza mbegu za mahindi
Ruvu Shooting yazindukia Musoma