Wakala wa mbegu bora za kilimo nchini ASA imesema kwamba msimu wa kilimo 2021/2022 imekusudia kusambaza tani 500 za mbegu bora za mahindi kwa kanda ya ziwa na Magharibi ili wakulima wafa nyae maandalizi ya msimu mapema.

Hayo yamesemwa na meneja wa shamba la mbegu bora za kilimo la kilimi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora Jacob Chiwanga wakati akipokea tani 80 a mbegu katika kituo cha reli Tabora.

Chiwanga amesema kuwa ASA kwa kanda ya ziwa na magharibi itasambaza mbegu kwa njia ya reli ili kupunguza gharama za usafiri kwakuwa usafiri wa reli ni rahisi tofauti na kukodi magari.

“Tani hizo 80 kama wangetumia usafiri wa malori yangetumika  zaidi ya magari 8 ya tani kumi   jambo ambalo Gharama zingeogezeka mara dufu”Amesema Chiwanga.

Amesema kwa upande wa Wilaya na mikoa ambayo ipo kando ya barabara kuu ya kanda  wataendelea kusafirisha kwa magari ambapo hadi sasa wamesha sambaza tani 30 katika wilaya za Igunga ,Nzega na upande wa mikoa ya ziwa.

Watuhumiwa 305 wakamatwa kwa makosa mbalimbali
Meddie Kagere azima minong'ono