Jeshi la Polisi mkoani Tabora limefakiwa kuwakamata watuhumiwa  305 wa kamakosa mbalimbali ya uhalifu kwa kipindi cha Januari hadi  Septemba mwaka huu

Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia misako mbalimbali inayoendeshwa na jeshi hilo katika wilaya zote 7 za Tabora ambapo watuhumiwa 127 wa kamaso ya vunjaji ,105 wa makosa ya mauaji na 73 ya ujambazi .

Akizungumza na waadishi wa habari ofisni kwake kamanda wa polisi mkoani Tabora, Safia Jongo  amesema kuwa matukio hayo yamekuwa ni kunzia januari hadi setemba mwaka huu, ambapo wamefanikiwa kukamata silaha 54 ambazo ni AK.47 ,1,Gobole 30,Risasi 5,Shourtgun 13 na Bastola zilizotengenezwa kienyeji 11 na mitambo 5.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani Tabora limemkamata mtuhumiwa mmoja katika kitongoji cha Miyenga Kijiji cha Mwakashidye kata ya Ibiri Wilaya ya Uyi Mkoani Tabora, akiwa na magunia ya bangi 19 na vifurushi 3 vya akiwa na gunia moja la mbegu za bangi ndani ya nyumba yake.

Sambamba na hayo yote Kamanda Jongo ametoa onyo kwa waganga wa kienyeji ambao hawana vibali vya kufanya shughuli zao lazima wafate utaratibu uliowekwa na serikali,kwani wao ndio chanzo cha kuleta mauaji kwa kupiga ramli chonganishi watakamatwa na kufikishwa Mahakamani.

Hata hivyo Jeshi hilo linaendelea kutoa tahadhali ya kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona (UVICO 19) kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono na sabuni kwa maji tiririka na kutumia vitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko isikuwa ya lazima.

Habari Picha:Rais Samia akishiriki maadhimisho ya siku yamlezi wa Skauti
ASA waanza kusambaza mbegu za mahindi