Lionel Messi alifunga bao lake la 100 katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya wakati Barcelona ikiibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Olympiakos.
Licha ya Barcelona kucheza pungufu baada ya Gerard Pique kupewa kadi nyekundu walitawala mchezo huo na kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 1-0 kufuatia bao la kujifunga la Nikolaou dakika ya 18.
Barca walianza kipindi cha pili kwa kasi na mnamo dakika ya 61 Lionel Messi alipachika bao la pili kwa kupiga mpira wa adhabu uliotumbukia kimiani moja kwa moja, bao hilo likiwa ni la 100 katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
-
Antonio Conte na Jose Mourinho watupiana vijembe
-
Jose Mourinho aikana kauli yake
-
Aliou Cisse apingana na ripoti ya Liverpool, amuita Mane
Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 30 alimpatia pasi Lucas Digne aliyefunga bao la tatu kabla ya Dimitris Nikolaou kuipatia Olympiakos bao la kufuta machozi dakika ya 89.
Katika mchzo huo Gerard Pique alipewa kadi pili ya njano na kutolewa nje baada ya kutumia mkono kufunga bao dakika ya 42 ya mchezo huo.
Katika michezo mingine Marcus Rashford jana alifunga bao pekee katika mchezo wa Champions League dhidi ya Benfica na kuiweka United kileleni mwa kundi lao lakini mchezaji huyo ameingia kwenye kundi la majeruhi la Paul Pogba, Eric Bailly na Morouane Fellaini baada ya hapo jana kuumia.
Chelsea pia walikuwa dimbani Stamford Bridge kuwakaribisha As Roma ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kufungana mabao 3-3.