Meneja wa mashetani wekundu (Manchester United) Jose Mourinho amekanusha uvumi unaoendelea kusambaa, kwa kudai huenda akaondoka Old Trafford na kuhamia jijini Paris kwenda kukinoa kikosi cha SG.

Mourinho aliibua uvumi huo kufuatia kauli yake aliyoitoa mwishoni mwa juma lililopita, ambapo alisema hatomaliza kazi yake kama mkuu wa benchi la ufundi huo Old Trafford, kutokana na hitaji la kutaka kufanya mambo mapya.

Alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliokua unazungumzia mchezo wa ligi ya mabingw abarani Ulaya utakaochezwa hii leo kati ya kikosi chake dhidi ya SL Benfica,  Mourinho alisema hakuna ukweli wowote kuhusu mpango wa kutaka kuhamia PSG.

”Sitatia saini kandarasi ya miaka mitano na kwamba sitohamia PSG”, alisema Mourinho mwenye umri wa miaka 54.

”Kwa sababu kwa siku moja ninaambiwa kwamba nitatia saini kandarasi ya miaka mitano ulio na thamani ya Pauni bilioni moja  na siku nyengine mkasema kuwa ninaondoka na kuelekea PSG”.

Katika mahojiano ya Jumapili, Mourinho ambaye aliisifu klabu hiyo ya Ufaransa, kufautia mwanae kupenda kwenda kutazama michezo ya PSG badala ya ile ya Manchester United.

Kwa nini Paris? Kwa kuwa kuna kitu maalum. Mchezo mzuri, ubora, ujana ni vitu vya ajabu, alisema.

Nadhani hilo ndio jibu, hakuna kinachofanyika. Mourinho ambaye yuko katika msimu wake wa pili na Man Utd hajawahi kufanya kazi kwa zaidi ya miaka minne katika klabu moja.

Mfalme wa Oman aunga mkono juhudi za JPM
Ghana yachanja mbuga FIFA U17, kupambana na Mali