Timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji wao nyota Lionel Messi wako hatarini kukosa kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu 1970 baada ya kutoka sare tasa na Peru.
Timu nne pekee kutoka bara la Amerika Kusini ndizo zitakazo fuzu katika michuano hiyo itakayofanyika Urusi mwaka 2018.
Hadi sasa Argentina ambo ni mabingwa wa kombe la dunia mara mbili wapo nafasi ya sita wakiwa wamesalia na mchezo mmoja pekee na watalazimika kushinda mchezo huo wa mwisho dhidi ya Ecuador kubaki katika nafasi ya tano, ili wacheze michezo miwili ya mchujo dhidi ya New Zealand.
-
Video: Ujerumani yafuzu kombe la dunia 2018
-
Kane aipeleka Uingereza kombe la dunia
-
Pogba marufuku kucheza mpira wa kikapu
Timu zote katika kundi la Amerika ya Kusini zimecheza michezo 17 na Brazili wanaogoza kwa pointi 38,Uruguay pointi 28 ,Chile pointi 26, Colombia pointi 26, Peru pointi 25 na Argentina wapo katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 25.
Kocha wa Argentina Jorge Sampaoli amekiri kwamba mambo sio mazuri lakini ameongeza kwamba ana imani kuwa iwapo timu hiyo itacheza ilivyocheza dhidi ya Peru, basi watafuzu kwa Kombe la Dunia. Mechi za mwisho zitachezwaJumatano mnamo Oktoba 11.