Muimbaji wa kike ambaye ni kati ya wasanii wachache wa kike wapya walioingia kwenye ‘Orodha A’ ya wasanii nchini, Lulu Diva amekanusha taarifa za kutumia ‘kitaulo’ au mkorogo kubadili rangi yake.

Mrembo huyo ambaye anatamba na wimbo wake wa ‘Utamu’ amesema kuwa mabadiliko ya rangi yametokana na hali ya asili na hakuna mkorogo uliotumika kufanya mabadiliko hayo kama baadhi walivyomkosoa.

Akizungumza na EATV, Diva huyo wa Bongo Fleva amesema anatambua madhara anayoweza kuyapata endapo atatumia vipodozi hivyo.

“Hapana, mimi sijapiga kitaulo nakataa. Unajua Mimi kwetu Zanzibar sasa unajua watu wa Pemba wengi ni weupe na weusi ni wachache. Hii ni rangi yangu,” Lulu Diva alifunguka.

“Jamani watu wasijichubue ili wawe na rangi kama Lulu Diva, my dear wataungua,”  aliongeza.

Alisema siri ya urembo na rangi yake ni kula mbogamboga na kunywa maji mengi.

 

Messi hatarini kukosa kombe la dunia 2018
Bulaya: Ninafuatiliwa na watu waliovaa mavazi ya kininja