Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Jamal Malinzi jana Novemba 15, 2016 alimtembelea Mstahiki Meya wa Jiji la Seongnam, Jae-myung Lee na kumshukuru kwa namna ambavyo ameipokea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).

Serengeti Boys waliopo Korea Kusini kwa michezo ya kirafiki ya kimataifa ambako Jiji la Seongnam ni mshirika wa klabu ya Seongnam FC ambao ndio wenyeji wa timu yetu ya vijana ambayo ilifanya michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki.

Katika mazungumzo Meya huyo, aliihakikishia TFF kuwa jiji lake litaendelea kushirikiana na shirikisho katika kuendeleza soka la vijana wakike na wakiume.

Katika kumtembelea Meya huyo, Rais Malinzi aliambatana na Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na benchi nzima la ufundi, linaloongozwa na Kocha Bakari Nyundo Shime na msaidizi wake, Muharami Mohammed Sultan pamoja na Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya soka la vijana, Kim Poulsen.

Baadae jioni ya Novemba 15, 2016 Rais Malinzi alikutana na Rais wa Shirikisho la soka la Korea Kusini (KFA), Chung Mong-Gyu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Hyundai.

Rais wa KFA Mong-Gyu naye alihakikishia TFF kuwa Shirikisho la soka la Korea litasaidia kuendeleza soka la vijana Tanzania sambamba na kusaidia mafunzo ya makocha.

TFF Yampiga Marufuku Christopher Mahanga
Rafael Varane Azima Ndoto Za Jose Mourinho