Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Julai,2017 umepungua hadi kufikia asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 5.4 iliyokuwa mwezi juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii jijini Dar es salaam, Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kupunguwa kwa mfumuko wa bei wa mwezi julai 2017 kumechangiwa hasa na kupunguwa kwa bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi julai,2017 zikilinganishwa na bei za mwezi julai,2016.

Amesema kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na Nyama kwa asilimia 3.8, samaki wabichi asilimia 14.1, dagaa kwa asilimia 8.4, kabichi kwa asilimia 16.6, iringanya kwa asilimia 10.6, vitunguu kwa asilimia 13.2, karoti kwa asilimia 16.9,njegere kwa asilimia 15.7 na viazi mviringo kwa asilimia  13.5.

Vile vile, Kwesigabo amesma kuwa thamani ya shilingi ya Tanzania imezidi kuimarika ambapo uwezo wa shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 91 na senti 87 mwezi julai, 2017 ikilinganishwa na shilingi 91 na 66 iliyokuwa mwezi juni.

Aidha, ameongeza kuwa mfumuko wa bei nchini unamwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi julai,2017 umepungua hadi asiliia 7.47 kutoka asilimia 9.21 mwezi juni,2017.

Hata hivyo, Mfumuko huo wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini

Majaliwa apiga marufuku ununuzi wa Tumbaku kwa dola
Video: Bilionea Bill Gates aonekana Tanga, Manji hatarini kufunguliwa kesi nyingine