Baraza la Madiwani Halmashuri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro kwa kauli moja limeadhimiwa kumshusha cheo Mganga mkuu wa Wilaya hiyo, Dastan Mshana kwa Kosa la Kutumia Madaraka vibaya kwa kununua kopyuta nane chakavu kinyume na sheria za manunuzi.

Makamu mwenyekiti Baraza la Madiwani Wilaya ya Gairo, Clemence Msulwa amesema baada ya kufanya uchunguzi wamebaini Mganga huyo mkuu pia alifoji sahini ya madereva na kuchukua mafuta ya lita 100 na kuyatumia kwa matumizi binafsi.

Amewataja wengine waliohusika katika sakata Hilo kuwa ni Afisa Habari wa Halmshauri ya Wilaya ya Gairo, Cosmas Njingo, Afisa TEHAMA daraja la pili, Godfrey Lupembe na dakatari Ruben Mfugali.

Watumishi hao, waliohusika katika tukio hilo wote kwa pamoja wamepewa adhabu ya kukatwa mishahara yao kwa asilimia 15 kwa kipindi cha miaka mitatu na kutakiwa kushirikina kununua kopyuta hizo mpya, huku Mkuu wa wilaya ya Gairo, Jabir Makame akiwataka wafanyakazi kuwa waadilifu.

Nyumba yateketea, 35 wanusurika kifo
Polisi yamzidi ujanja 'Mafia' dawa za kulevya