Jumla ya Watu 35 wamenusurika kifo, baada ya nyumba wanaishi kuteketea kwa Moto majira ya usiku wa kuamkia Septemba 12, 2022 Mkoani Morogoro.

Wakiongea mara baada ya tukio hilo, baadhi ya wapangaji wa nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Makaburi “C ” kata ya Mji mpya Manispaa ya Morogoro wamesema Moto huo ulianza kuwaka katika moja ya swichi ya umeme kisha kusambaa nyumba nzima na kupelekea madhila hayo.

Nyumba iliyopo mtaa wa Makaburi “C ” kata ya Mji mpya Manispaa ya Morogoro ikiteketea kwa moto, watu 35 walinusurika kifo.

Mwakilishi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa Morogoro, Sajenti Mpango Funga amesema hadi sasa bado chanzo cha Moto huo hakijafahamika na kudai kuwa hakuna madhara kwa binadamu lakini mali zote zimeteketea.

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro hakuweza kupatikana mara moja ili kuthibitisha tukio hilo na kujua thamani halisi ya mali zilizoteketea ingawa inaarifiwa kuwa hakuna majeruhi wala vifo.

GGM Ladies yawapa malezi ya kitaaluma Wanafunzi wa kike
Mganga Mkuu ashushwa cheo kwa kununua vifaa chakavu