Mapigano yameripotiwa katika eneo la mpaka lililo na utata wa umiliki la al-Fashaga kati ya jeshi la Sudan na lile la Ethiopia kufuatia madai ya kukamatwa, kunyongwa na kuonyesha hadharani miili ya Wanajeshi saba na raia mmoja aliyeuawa mwishoni mwa juma.

Afisa Mkuu wa Usalama katika eneo la Amhara nchini Ethiopia, Assefa Ashege amesema Jumanne Juni 28, 2022 Sudan ilirusha silaha nzito na kutwaa tena maeneo yake kadhaa yaliyokuwa yakishikiliwa na jeshi la Ethiopia, kwa kufyatua mizinga ya masafa marefu lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Ugomvi wa hivi punde, kuhusu al-Fashaqa, ambapo kaskazini-magharibi mwa mkoa wa Amhara nchini Ethiopia unakutana na tatizo la chakula linaloikabili Sudan katika jimbo la Gedaref ambalo limekuwa likitatuliwa na wakulima wa Ethiopia kwa miongo kadhaa, pamoja na mzozo wa kidiplomasia kuhusu ujenzi wa Ethiopia wa bwawa la kufua umeme.

Maafisa wa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa wamekanusha madai ya Sudan ya wanajeshi wake kuwakamata na kuwanyonga wanajeshi saba wa Sudan, Lakini pia imesisitiza na kuwashutumu wanajeshi wa Sudan kwa kuvamia ardhi yake.

Mapema siku ya Jumanne wiki hii, kundi linalojumuisha wanaharakati na waandishi wa habari walikusanyika mbele ya ubalozi wa Ethiopia katika mji mkuu Khartoum, wakiwa na mabango yenye maandishi “Fashaqa ni ya Sudan”.

Kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili za Afrika, ambazo pia zinakabiliwa na mzozo wa Ethiopia kujaza bwawa kubwa la kuzalisha umeme kando ya Mto Nile, kumeibua wasiwasi juu ya usalama na utulivu katika eneo la Afrika mashariki, ambako Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda zimeongezeka.

Hujaji afariki Makka, Saudi Arabia
Gabriel Jesus: Chanzo ni msichana aliyenidharau