Kampuni ya Datavision International tayari imeadhimisha kumbukizi ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, ambapo imepanda miti katika Shule ya Msingi Boma, iliyopo Wilaya ya Ilala Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa kuweka alama za kukumbukwa katika jamii.

Akizungumza wakati wa sherehe hizo Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo William Kihula amesema Datavision inajivunia kuwa sehemu muhumu ya jamii na Serikali, na imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa jamii kupitia kampuni zake tanzu.

Amesema, “Kama sehemu ya jamii tumeona ni vyema tunaposheherekea miaka 25 ya tangu kuanzishwa kwa Datavision tukapanda miti katika shule hii ili kuweka alama kwa wanafunzi hapa pamoja na kutekeleza kwa vitendo mpango wa utunzaji mazingira.”

“Tunaamini miti hii itatunzwa na tutaiona ikiwa imekuwa Datavision itakapotimiza miaka 50 na vizazi vitakavyokuwepo watajivunia tukio hili la leo,” alibainisha Kihula.

Nao baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Boma ilipopandwa miti hiyo, wameishukuru kampuni ya Datavision kwa kuchagua kupanda miti ya matunda na kivuli kwenye shule hiyo na kuahidi kuitunza miti hiyo.

Datavision International, ilianzishwa rasmi Oktoba 27, 1998 ikibobea katika masuala ya tafiti na takwimu Duniani na zifuatazi ni baadhi ya Picha zikionesha matukio mbalimbali wakati wa zoezi la upandaji Miche ya Miti katika Shule ya Msingi Ilala Boma, jijini Dar es Salaam.

Balozi, Profesa wapanga kuimarisha usalama wa kikanda
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 28, 2023