Shirika la ndege la Ethiopia nchini Nigeria limepiga marufuku mikoba iliyopewa jina la utani “Ghana Must Go” kutoka kwa safari zao za ndege, mifuko  hiyo ilipata jina la utani nchini Nigeria katika miaka ya 1980, wakati maelfu ya wahamiaji wasio na vibali waliobebea mifuko hiyo, wengi wao wakiwa Waghana, walifukuzwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Shirika hilo la ndege inasema wabebaji wa mifuko hiyo, inayopendwa na wafanyabiashara, inaweza kuathiri vibaya vifaa vya uwanja wa ndege.

“Marufuku hiyo ilianzishwa kwa sababu ya kutokea mara kwa mara kwa uharibifu wa mikanda ya kusafirisha mizigo katika viwanja mbalimbali vya ndege, na kusababisha gharama kubwa kwa mashirika ya ndege husika“.

Wameongeza kuwa, mifuko hiyo inaweza kutumika ikiwa ingepakiwa vya kutosha kwenye katoni au kontena gumu la mstatili.

Ethiopia Airlines hufanya safari za ndani na kikanda nje ya kitovu cha kibiashara cha Nigeria, Lagos.

Mifuko hiyo ni maarufu sana kote barani Afrika, na sehemu kubwa ya dunia, na inaonekana katika viwanja vya ndege vingi.

Mifuko hii inamajina  tofauti katika meneo mengi kwamfamo Nchini Kenya, inajulikana kama mifuko ya Nigeria, huku nchini Tanzania ikijulikana kwa jina la Shangazi kaja na Wazimbabwe wanaiita mifuko ya Botswana.

Mnamo mwaka wa 2017 KLM na Air France, waliweka marufuku kwa sababu walisema mifuko hiyo inaweza kutanua na kuziba mifumo ya utoaji mizigo.

Silaa: Hakuna huruma wanaovunja sheria kipindi cha Uchaguzi
Wanaume pimeni VVU - Majaliwa