Naibu Waziri wa mambo ya ndani, Jumanne Sagini amesema Serikali imeshatoa maelekezo kwa wakuu wote wa Mikoa ambao ni wenyeviti wa ulinzi na usalama kuwa na mipango ya usimamizi wa matumizi bora ya ardhi kwa kuwapanga wakulima na wafugaji ili kuepuka muingiliano unaosababisha mogogoro.

Segini ameyasema hayo hii leo Aprili 28, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Kilwa Kusini Ally Kasinge, aliyehoji ni keanini bado migogo ya wakulima na wafugaji inaendelea na nini jukumu la Jeshi la Polisi kuzuia na kukomesha jambo hilo badala ya kuendelea na kesi ambayo hatma yake huwa sio nzuri.

Naibu Waziri wa mambo ya ndani, Jumanne Segini.

Amesema, Jeshi la polisi kupitia kitengo cha Polisi jamii wanaendelea kuelimisha wananchi kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima nankuongeza kuwa, “tuwaombe wataalamu wetu wa ngazi za Serikali za mitaa ambao hufanya tathimini ya uharibifu wa mazao kabala Polisi hawajachukua hatua za kusajili kesi Mahakamani watimize wajibu wao ipasavyo.”

Aidha ameshauri kutumia miundombinu iliyopo ya upatanisho kati ya wakulima na wafugaji hali ambayo inaweza kusaidia kupunguza na hatimaye kuondoa sintofahamu ambazo hutokea mara kwa mara na kuziingiza pande hizo mbili katika maelewano mabovu na migogoro isiyoisha.

Ngassa azishauri Simba SC, Young Africans
Mchungaji mbaroni kwa matukio 98