Kutoka nchini Malawi, Serikali ya nchi hiyo imemtumia maombi bondia mkongwe Mike Tyson ikimuomba kuwa balozi wa zao la bangi inayozalishwa nchini humo.

Ombi hilo limetoka kwa Waziri wa Kilimo wa nchini hiyo  Lobin Lowe  ambaye ameweka wazi kuwa kuhalalishwa kwa zao la bangi nchini humo mapema mwaka jana kumetoa fursa nyingi, huku dhumuni kubwa ni zao hilo kutumika kama Dawa nk.

“Pamoja na Faida kadhaa zenye kuonekana, Malawi inaweza Kutokwenda peke yake kwa kuwa sekta  hii si rahisi, Inayohitaji ushirikiano mkubwa, kwa hiyo ningependa kuomba/kukuchagua Bw. Mike Tyson kuwa kama balozi bangi inayozalishwa Malawi” – aliandika waziri huyo.

Pamoja na hayo inaelezwa kuwa Mike Tyson kuna uhusiano kidogo kati ya Mike Tyson na nchi ya Malawi na kuwa alipaswa kuwa nchini humo tangu wiki moja iliyopita, ila safari yake ilisimamama kwa muda kutokana na serikali ya nchi hiyo kuwa haikukamulisha kwa wakati maandalizi ya kumpokea Mwana madumbwi huyo mkonge.

Rolls-Royces waibuka na ndege ya umeme yenye kasi zaidi
Ummy atangaza waliochanguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2022