Jumamosi (Mei 20 ilikuwa ngumu kwa mashabiki wa Arsenal baada ya timu kupokea cha yao kichapo bao 1-0 na kuitawaza rasmi Manchester City kuwa  mabingwa wa ligi ya England kwa msimu huu 2022/23.

Meneja wa Klabu hiyo ya jijini London raia wa Hispania, Mikel Arteta amefunguka sababu ambazo zimeiangusha timu hii iliyokuwa ikipewa zaidi ya asilimia 70 za kuchukua ubingwa.

Taji linakuwa ni la sita kwa Manchester City na la tatu mfululizo na imekuwa timu ya tano kuweka hili rekodi hiyo baada ya Huddersfield Town, Arsenal, Liverpool na Manchester United (mara mbili).

Man City imetwaa ubingwa ikiwa na pointi 85, huku ikiwa imebakiwa na mechi tatu kabla ya kumaliza ligi, jambo ambalo halikutegemewa na watu wengi kutokana na aina ya ushindani ambao Arsenal iliuonyesha tangu kuanza msimu huu.

Akizungumza baada ya kichapo kutoka kwa Nottingham Forest, Arteta amesema moja ya sababu zilizochangia kufikia hatua waliyonayo kwa sasa ni kubadilika kwenye namna ya kuzuia na kuruhusu mabao kirahisi.

“Inauma kuona tumepambana kwa miezi 11 ili kutwaa ubingwa, lakini mwisho tumepoteza, nafikiri tulistahili kupata tulichopata kwa namna tulivyocheza katika mechi zetu za mwisho,” amesema kocha huyo.

Amesema kila walipokuwa wanakaribia mwisho wa ligi ndipo wachezaji wake walikuwa wanapunguza ubora wao tofauti na ilivyokuwa mwanzini.

Upepo mbaya ambao uliipitia Arsenal kwenye mechi zao saba za hivi karibuni ndiyo ulioipa Man City nafasi ya kupanda kwenye kilele cha msimamo hadi kufikia kutwaa taji hili.

Arsenal ilianza gundu baada ya kutoka sare dhidi ya Liverpool, West Ham na Southampton kabla ya kufumuliwa kwa mabao 4-1 dhidi ya Manchester City na baadaye kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Brighton.

Matokeo haya yaliiwezesha Man City kupanda kileleni kwa pointi 85 na baada ya hapo Arsenal imeshinda mechi mbili dhidi ya Chelsea na Newcastle, lakini bado imeendelea kusalia kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 81, baada ya kucheza mechi 36.

Baada ya kucheza dhidi ya Nottingham Forest jana, Arsenal imebakisha mechi moja ambayo itacheza Mei 28, dhidi ya Wolves saa 12:30 jioni.

Kashfa ya Sukari: Vigogo, wafanyabiashara kizimbani
Prof. Mbarawa ataja vipaumbele kumi sekta ya Uchukuzi