Na Mwandishi Wetu, Geita.

Mambo bado yanadaiwa kuonekana kuwa magumu kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, baada ya kuahirisha mkutano wake kutokana na kukosa watu katika Kijiji cha Ilolangula, Wilayani Mbogwe Mkoani Geita.

Mkutano wa Lissu ulipangwa kufanyika katika Kijiji hicho, kama sehemu ya mwendelezo wa ajenda ya mikutano yao inayofanyika Kanda ya Ziwa ambapo inadaiwa kuwa Lissu aliingia kijijini hapo na timu yake kwa ajili ya mkutano huo.

Aidha, katika hali ambayo haikutarajiwa, aliamua kuahirisha kuendelea na mkutano wake ikidaiwa kuwa ilikuwa ni njia ya kuepuka aibu anayokutana nayo kama mwendelezo wa mikutano yao inayoonekana kukosa mvuto.

CHADEMA, wamezindua ziara za mikoani wakianzia na mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo hata hivyo imekuwa na mahudhurio yasiyoridhisha, huku chanzo cha hali hiyo kikitafsiriwa kama wananchi kuchukizwa na mwenendo wa Lissu kutoa lugha za kuudhi wakati wa hotuba zake.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 2, 2023
Lukaku avuruga mpango wa usajili