Kocha wa zamani wa klabu za Azam FC, Ndanda FC na Mbeya City Meja Mstaafu Abdul Mingane, ameupongeza Uongozi wa Simba SC na Benchi la Ufundi la klabu hiyo kwa kucheza michezo miwili ya Kimataifa ya Kirafiki.

Simba SC ilikitumia kipindi cha mapumziko ya Ligi Kuu Msimu huu, kuchezo michezo ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Asante Kotoko (Ghana) na Al Hilal (Sudan) kwenye Michuano maalum iliyopigwa nchini Sudan.

Kocha Mingange amesema michezo hiyo itakisaidia kikosi cha Simba SC kuelekea Michuano ya Kimataifa ambayo itaanza rasmi mwishoni mwa juma liljalo, ambapo Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania Bara watakipiga dhidi ya Mabingwa wa Malawi Nyasa Big Bullet.

“Ni Michezo ambayo itamsaidia zaidi kocha kujipanga kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa ukiachana na zile ambazo amecheza za ndani na nje ya nchi.”

“Mchezo na KMC utamuongezea ubora kwenye kikosi kabla ya kwenda Malawi, siku tatu kabla ya mchezo wa Kimataifa dhidi ya Big Bullet, naamini siku hizo zinawatosha kabisa.” amesema Mingange

Kwenye Michuano ya Kimataifa ya Kirafiki, Simba SC iliifunga Asante Kotoko ya Ghana 4-2 kabla ya kupoteza kwa 1-0 dhidi ya wenyeji Al Hilal jana Jumatano (Agosti 31).

Simba SC inatarajia kurejea jijini Dar es salaam leo Alhamis (Septemba Mosi) ikitokea Sudan, huku Jumamosi (Septemba 03) ikitarajia kucheza mchezo mwingine wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Arta Solar ya Djibout.

Zoran Maki: Michezo ya Sudan imetuimarisha
Dkt. Mabula: Wananchi hawamudu gharama za nyumba