Hatimaye Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly wamemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Jose Luis Miquissone, akitokea kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Miquissone amejiunga na miamba hiyo ya soka Barani Afrika kwa ada ya uhamisho inayotajwa kufikia Dola za Kimarekani laki tisa ($900,000) ambazo ni zaidi bilioni 2 kwa pesa za Tanzania.

Ada hiyo ya uhamisho inamfanya Miquissone kuweka Rekodi ya kuwa mchezaji alieuzwa kwa pesa nyingi zaidi kwenye historia ya Soka la Bongo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, alionesha kiwango cha hali juu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika akiwa na Simba SC, huku akifunga bao la ushindi dhidi ya Al Ahly timu hizo zilipokutana jijini Dar es salaam.

Mlipuko wasikika nje ya uwanja wa ndege Kabul
TPRI yakamata kiuatilifu bandia chupa 140