Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ameidhinisha kwa kupitisha sheria mpya nchini humo inayoipa serikali mamlaka ya kuziondoa hewani tovuti ambazo ni tishio kwa usalama na uchumi wa nchi hiyo.

Gazeti la serikali Al-Ahram limesema kuwa, sheria hiyo imebeba pia adhabu kali kwa wadukuzi wa mifumo ya serikali ambao unawabana watu kutumia mtandao kwa kiwango kikubwa.

Shirika la kufuatilia uhuru wa kutoa maoni na kujieleza la ”Association of Freedom of Thought and Expression” lenye ofisi zake jijini Cairo limesema kuwa, takribani tovuti 500 zimezuiliwa kupatikana nchini humo (blocked) kwa amri ya serikali tangu mwezi Mei mwaka 2017.

Mamlaka imesema kwamba hatua mpya zitahitajikia ili kukabiliana na ugaidi na vurugu za aina yeyote.

Makundi ya kutetea haki za binadamu zimeishutumu serikali kwa kujaribu kuwanyima haki wapinzani.

Mwezi uliopita mswada mwingine ulipitishwa na bunge la nchi hiyo lakini bado rais Sisi hajaupitisha unaodai kuwa mtu yeyote ambaye ana marafiki zaidi ya 5,000 kwenye mtandao wa kijamii inabidi awe kwenye uangalizi maalum na  tovuti yake itachukuliwa kama tovuti ya kuhabarisha umma na maudhui yake yatafuatiliwa na serikali.

Watakaovunja sheria hizi mpya wanakabiliwa na faini ya zaidi ya shilingi milioni 22 za Kitanzania, au kifungo gerezani au vyote kwa pamoja.

Hata hivyo Nchi hiyo baada ya kufungia maandamano mitandao ya kijamii ilikuwa inatumika kama sehemu pekee ya kuikosoa serikali ya Misri.

Mwezi uliopita Sheria ya haki za binadamu ”Human rights watch” ilitoa angalizo mara baada ya mamlaka ya taifa hilo kuanza kuwafungulia kesi wanaharakati waandishi wa habari na yeyote ambaye atakosoa nchi hiyo.

Hata hivyo Serikali ya el-Sisi ambaye aliingia madarakani mwaka 2014, imekosolewa vikali kwa kuendelea kukandamiza uhuru wa habari na maoni nchini humo.

 

 

 

Video: Matamasha ya Kustaajabisha zaidi Duniani
Mwanafunzi kidato cha 4 auawa kikatili, 'achunwa ngozi'