Miss Tanzania 2016, Diana Edward Lukumai ambaye pia ni kiongozi wa kampeni ya kukomesha ukeketaji katika jamii ya kimasai inayojulikana kama Masaai dondosha wembe, Leo amevutiwa kutembelea kituo cha walemavu cha ‘Mitwe Charitable Foundation’ kilichopo karibu na Msikiti wa Magomeni Mwembechai na kukabidhi vifaa mbalimbali kutoka kwa wasamalia wema walioguswa na matatiz0 ya walemavu hao.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Fimbo, kiti cha kutembelea walemavu wa miguu ‘wheelchair’ pamoja na kutoa ushauri kwa walemavu hao.
Walemavu nao walitoa shukrani na kuwaomba wasamalia wema wasichoke kuwasaidia kwani hawana watu wa kuwasaidia, wanawake wanahitaji ajira, mabinti wadogo wanahitaji kusoma, kipato chao hakitoshi kutokana na kushindwa kufanya kazi zitazowaingizia kipato cha kuwawezesha kukidhi mahitaji ya familia zao na hivyo waliomba kila mmoja katika nafsi yake ajitoe katika hili kwa kutoa msaada.
Diana alieleza kwa yeyote atakaye guswa na kuhitaji kutoa msaada kwa ajili ya walemavu hawa, awasiliane naye ili aunganishwe na Mwenyekiti wa chama chao cha walemavu kutatua tatizo hilo.
”Tunaweza kuwasaidia walemavu hawa ili mwisho wa siku waweze kujikimu kimaisha, NGO’s na wasamalia wengine tuungane kuwasaidia watu wa aina hii katika maeneo tunayoishi. Kidogo cha kwangu cha kwako na cha yule kwa pamoja kitawapa faraja watu hawa”, alisema Diana.
Diana aliwasilisha ujumbe huo kupitia mitandao yake ya kijamii.