Mabondia Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumzia mpambano huo, mratibu Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema kuwa amewasainisha mabondia hao kwa kuwa viwango vyao vipo juu sana katika kipindi hiki ambapo anaamini utakua mpambano mkali wa kufungua mwaka 2016

Super D, ameongeza kwa kusema mbali na mpambano huo, pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia mbalimbali watapanda ulingoni.

Mohamed Matumla, atavaana na Cosmas Cheka wakati mabondia Mada Maugo atavaana na Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati yao pia bondia Vicent Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa Morogoro atamenyana na Seba Temba

Super D amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kwa wingi kushudia mapambano hayo ambayo yatakua na msisimko wa aina yake.

Amesema wamepanga kuanza ngumi hizo mapema ili wapenzi wawahi kurejea sehemu za makazi yao kuendelea na furaha ya sikuku ya pasaka, na kujumuika na familia zao.

Unataka kumjua mchawi wako kazini? Soma hapa
Mabingwa Wa Tanzania Bara Kuwafuata Sekho De Joackim