Shirika la afya Duniani, WHO limezindua mkakati mpya wa kukabiliana na dharura ya tatizo la usugu wa dawa dhidi ya ugonjwa wa Malaria Barani Afrika.
Taarifa ya WHO, iliyotolewa jijini Geneva Uswisi imesema mkakati huo unazinduliwa wakati huu ambapo wiki ya kuelimisha kuhusu vijiua vijiumbe maradhi ikianza hii leo Novemba 18 – 24, 2022 ukiwa na lengo lengo la kuongeza uelewa wa ongezeko la usugu wa viuavijasumu na dawa nyingine.
WHO inasema, katika miaka ya hivi karibuni kumekuweko na taarifa kutoka barani Afrika ya kuibuka kwa vimelea vipya vya Malaria ambavyo havitibiki kwa dawa aina ya Artemisinin ambayo ndio dawa kuu na bora iliyoko hivi sasa kutibu Malaria.
Shirika hilo, pia linahofu kuwa vimelea katika baadhi ya maeneo barani humo vinagoma kutiibika na daw nyingine ambazo huchanganywa na Artemisinin na hivyo hatua thabiti vinapaswa kuchukuliwa kulinda ufanisi wa dawa hiyo.