Mke wa mtuhumiwa wa sakata la usafirishaji wa tumbili kinyemela kutoka nchini kuelekea nchini Armenia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ameripotiwa kufariki dunia kwa mshtuko baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa mumewe.

Taarifa za kifo cha mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Mariam Vardanyan ambaye ni mke wa mtuhumiwa raia wa Uholanzi, Artyom Vardanyan zilitolewa na Mkurugenzi wa Msaidizi wa Huduma ya Dharura wa Hospitali ya St. Grigor Manukyan ilithibitisha kuwa chanzo cha kifo chake ni mshtuko.

Taarifa hizo pia zimethibitishwa na wakili anayewatetea watuhumiwa wa kesi hiyo nchini, Kisak Mzava akibainisha kuwa chanzo cha kifo cha Mariam ni mshtuko uliotokana na taarifa za kukamatwa kwa mumewe.

Watuhumiwa wa Sakata hilo walikamatwa Machi 24 mwaka huu KIA wakituhumiwa kusafirisha tumbili 61. Hata hivyo, watuhumiwa wote bado hawajafikishwa katika mahakama yoyote nchini, wakiendelea kushikiliw na jeshi la Polisi.

Daraja la Juu ‘Flyover’ laporomoka na kuua makumi
Malinzi: Sitashangaa Hata Kesho Uwanja Wa Karume Nao Ukipigwa Mnada