Mkutano wa 60 Jumuiya ya Polisi wa kike Duniani IAWP umefungwa rasmi siku ya jana septemba, 2023 hapa New Zealand Auckland.

Katika ufungaji huo, wajumbe walishukuru kwa namna ambavyo Mkutano huo umewajenga kifkra na kuwaongezea maarifa mapya ambayo yataongeza chachu ya kiutendaji kutokana na mada mbalimbali zilizofundishwa katika Mkutano huo wa sitini.

Aidha wajumbe walipata fulsa ya kuonyesha Utamaduni zao ikiwa ni sehemu ya kutangaza tamaduni za kila nchi na kuonyesha tamaduni hizo Mkutano huo uliohudhuriwa na nchi sitini na tano kutoka bara la Ulaya na Afrika.

Ambapo Kamishna wa Polisi Utawala na rasilimali watu CP Suzan Kaganda amewaomba wajumbe wa IAWP kufika Nchini Tanzania kushuhudia vivutio vya utalii na tamaduni pamoja na mali kale zilizopo Tanzania bara na Zanzibar.

Aidha alibainisha kuwa anaamini watafurahi kuona namna Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na vivutio ambavyo havipo nchi nyingine duniani kama vile fuvu la binadamu wa kwanza olduvai George katika bonde Kreta ya Ngorongoro, ambapo New Zealand wamekabidhi Majukumu yote kwa Mkutano kwa ajili ya Mkutano ujao wa 61 IAWP, 2024 unaotegemea kufanyika Nchini Marekani jimbo la Chicago.

Robertinho: Miquissone anakuja mdogo mdogo
Daniel Levy: Tulikosea kumuajiri Mourinho, Conte