Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema mechi dhidi ya Algeria kuwania kucheza Kombe la Dunia, haitakuwa lelemama.

Mkwasa amesema wanajua kwamba itakuwa si kazi lahisi hata kidogo, lakini wanachotaka ni mafanikio. Stars itaivaa Algeria Novemba, mwaka huu.

“Ukitaka mabadiliko, lazima upambane. Kila mmoja anajua Algeria ni timu bora kabisa, lakini lazima tupambane ili kufanikiwa.

“Tunachoomba Watanzania watuunge mkono na sisi tutafanya kazi yetu kwa ufanisi mkubwa ili kuhakikisha tunafanikiwa,” alisema Mkwasa.

Stars imefikia hatua hiyo baada ya kuing’oa Malawi kwa jumla ya mabao 2-1.

Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Stars ilishinda kwa mabao 2-0, mechi ya pili ikalala kwa bao 1-0 mjini Blantyre, Malawi.

 

Algeria Yasababisha TFF Kuunda Kamati
Kuelekea Ufaransa 2016, UEFA Watoa Utaratibu