Mbunge wa jimbo la Kibamba, John Mnyika amekosoa mabadiliko yaliyofanywa na serikali kuihamisha Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu na kuwa chini ya Ofisi ya Rais.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Saranga katika jimbo lake, Mnyika alieleza kuwa uamuzi huo umelenga katika kuwabana wapinzani ambao sasa hivi wanaongoza halmashauri nyingi ili wasiwe huru kufanya maamuzi mbalimbali.

“Rais Magufuli amefanya kama alivyofanya Benjamini Mkapa wakati wa utawala wake kwa kutaka kutawala kibabe. Hatafika mbali kwa sababu ameshindwa kujenga mifumo thabiti, badala yake amebaki kuhimiza usafi wa siku moja,” alisema Mnyika.

Mnyika alimshauri rais John Magufuli kujenga misingi ya kujiendesha bila kutegemea msukumo kutoka kwake.

Himid Mao Azungumza Kilichowaponza Dhidi Ya Simba
Yanga Wapandwa Hasira Dhidi Ya Niyonzima