Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo Mnzava amesema Barabara kubwa za kuunganisha Tarafa za jimbo la Korogwe vijijini zimefunguka kutokana na ukarabati uliofanywa na kuondoa changamoto iliyokuwepo kutokana na jiografia ya eneo hilo iliyokuwa ikisababisha adha kwa wakazi wa maeneo hayo.

Mnzava ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media mjini Lushoto na kuongeza kuwa jimbo hilo lenye kata 29, kuna baadhi ya barabara zilikuwa hazipitiki kwa takribani miaka 10, 5 hadi 6 na kutokana na miundombinu yake kuharibiwa na mvua wakati wa masika na kutokukarabatiwa kwa muda mrefu.

Amesema, ”Jimbo letu ni kubwa lina kata 29 lakini pia limegawanyika sana, geografia yake ni ngumu na barabara nyingi bado ni za vumbi, na changarawawe kuna barabara zilikuwa hazipitiki kwa miaka 10, 6 hadi mitano lakini tunashukuru tangu mwaka 2020 mpaka sasa tumejitaidi karibu barabara zote kubwa za kufungua tarafa zote tatu zinapitika sasa hivi”

Mnzava ameongeza kuwa, ”Lutindi kulikuwa na barabara yenye changamoto sana tunaijenga kwa zege kwa kipindi hiki, tulikuwa na madaraja ambayo yalishindikana kwa zaidi ya miaka 10, daraja la makuyuni kwenda mswaa ambalo linatumia zaidi ya bilion 3.8 , na makandarasi yupo kazini na limefikia asilimia zaidi ya asilimia 60.”

Kuhusu changamoto ya maji ambayo ipo katika jimbo hilo, Mbunge huyo amesema tayari kuna miradi nane ambayo ikikamilika itatatua changamoto ya maji kwa wananchi wake na kwamba pia ipo miradi zaidi ya nane ambayo inaendelea katika maeneo tofauti ikigharimu shilingi bilion 4 na ikamilika itasaidia kupunguza changamoto ya maji kwenye jimbo hilo.

Morocco yajitoa Fainali za CHAN 2022
Kocha Mubiru aishangaa Mbeya City