Baadhi ya Waandishi wa Habari nchini, wamehuzunishwa na Kifo cha Mwanahabari mwenzao wa Gazeti la Nipashe la kampuni ya IPP Media, Richard Makore ambaye alifariki dunia katika ajali iliyoua watu 10 eneo la Ibanda Kona, lililopo Kata ya Kasamwa Wilaya na Mkoa wa Geita.

Makore alifariki Machi 7, 2023 baada ya basi la Sheraton lililokuwa likitokea jijini Mwanza kwenda Ushirombo Wilayani Geita, kupasuka tairi la mbele na kupinduka na kifo chake kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza – MPC, Edwin Soko.

Richard Makore.

Mbali na Waandishi mbalimbali kusikitishwa na taarifa hizo, pia taarifa ya MPC ilieleza kuwa, “MPC inasikitika kutangaza kifo cha Mwanachama wake Richard Makore kilichotokea kwenye ajali ya gari iliyotokea Mkoani Geita. Makore alikuwa anafanya kazi na Gazeti la Nipashe Mwanza na pia ni Mwanachama hai wa MPC.”

Aidha taarifa hiyo ilizidi kufafanua kuwa, “Kwa sasa mwili wake upo kwenye chumba cha kuhifadhi Maiti hospitali ya Geita. MPC inawaomba Wanachama wake wote kuwa watulivu kwenye wakati huu mgumu kwetu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.”

Pongezi kwa Wanawake Duniani - Dar24 Media
Tahadhari yatolewa utapiamlo kwa Watoto nchi nzima