Tahadhari ya tatizo la utapiamlo linalowaweka watoto nchini Malawi katika hatari kubwa ya kukumbwa na maradhi ya kipindupindu, imetolewa na Umoja wa Mataifa baada ya maradhi hayo kuenea maeneo mengi ya Taifa hilo.

Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto, UNICEF yameonyesha kuwa watoto wapatao milioni 4.8, sawa na nusu ya watoto wote katika nchi hiyo wanahitaji msaada wa kiutu.

Mtoto akipata vipimo kutoka kwa Muhudumu wa Afya. Picha ya EEAS.

Aidha, UN imesema hadi mwishoni mwa mwezi huu (Machi 2023), inatarajiwa kuwa watoto zaidi ya 213,000 watakumbwa na utapiamlo, huku 62,000 kati yao wakiweka katika kundi lenye hatari zaidi.

Hata hivyo, Afisa Mkazi wa UNICEF nchini Malawi, Rudolf Schwenk anasema mtoto anayesumbuliwa na utapiamlo yuko hatarini kufa kutokana na kipindupindu mara 11 zaidi ya mtoto mwenye afya njema.

MPC yathibitisha kifo cha Richard Makore, Waandishi wamlilia
Rais anataka mabadiliko sekta ya Mifugo: Majaliwa