Kufuatia maagizo aliyoyatoa wakati wa Ziara yake ya ukaguzi wa Mazingira ya hivi karibuni katika Bandari ya Dar es salaam, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amepokea ripoti kutoka kwa Uongozi wa Sumatra na Nemc ambao aliwaagiza kufuatilia maagizo aliyoyatoa mara baada ya ziara ya ukaguzi katika bandari hiyo.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Blandina Cheche imesema kuwa  Ofisi yake imepokea taarifa kutoka Mamlaka ya Bandari inayo onyesha aina na kiasi cha taka kinachozalishwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari – Machi.

Amesema kuwa ukaguzi maalumu kwa kutumia ndege umefanyika na kubaini kuwa hakuna uchafuzi uliobainika kufanywa na meli baharini katika kipindi husika na kuongeza kuwa jumla ya meli 79 za nje na 29 za ndani zimekaguliwa katika kipindi husika.

Kwa upande wake Meneja wa Leseni za Usafiri Barabarani (Sumatra), Leo Ngowi amesema kuwa Ofisi yake imeandaa mabango maalumu kwa ajili ya kusaidia kutoa elimu kwa umma juu ya namna bora ya matumizi ya vyoo kwenye barabara kuu na kuhamasisha Halmashauri na watu binafsi kujenga vyoo kwenye barabara kuu ili kuepusha uchafuzi wa mazingira.

Hata hivyo, Mpina ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuitisha kikao cha wadau wakiwemo Nemc, Wizara ya Afya, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya Kilimo, Mamlaka ya bandari pamoja na Sumatra ili kujadili namna bora ya usimamizi wa taka bandarini na katika vyombo vya usafiri nchi kavu.

 

Mbivu Na Mbichi Za Kipa Wa Mbao FC Kujulikana
Gianluigi Buffon: Tunaitaka Real Madrid Nusu Fainali