Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amemtaka mkandarasi anaeshughulika na ujenzi wa ukuta wa mto Pangani, Kampuni ya ( DEZO CIVIL CONSTRUCTION LTD ) kukamilisha ujenzi wa ufukwe wa huo kwa kipindi cha muda wa miezi kumi.

Ujenzi huo wa  sehemu ya ufukwe wa kaskazini ambao una urefu wa mita 950 ambazo kati yake mita 550 zipo katika ujenzi wa awali utagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 2.4, na unafadhiliwa na Mfuko wa nchi maskini zaidi duniani (LDCF), kupitia shirika la kimataifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira UNEP na Serikali ya Tanzania, kwa usimamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

Aidha, Katika ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi wa kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi katika fukwe za mto pangani Mkoani Tanga,  Mpina amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hayo ya mto pangani kuepuka uharibifu wa mazingira ya ufukwe huo kwa kupanda miche ya miti ya mikoko ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo wa kuhifadhi fukwe za  Mto Pangani,

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zubeda Abdalah amemuomba Mpina Kuiangali kwa jicho la pekee fukwe iliyoko katika maeneo ya Tanga DECO ambayo imeathirika kwa kiasi kikubwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia nchi na haipo katika bajeti ya kunusuru fukwe.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewaasa wasimamizi wa mradi huo kutumia fedha husika kwa matumizi kusudiwa  kama vile mafunzo ya upandaji, utunzaji na uendeleezaji wa mikoko kwa wana vikundi kwani imezoeleka huko nyuma kuwa fedha kama hizo zimekuwa zikitumika kwa matumizi yasiyo kusudiwa.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Wilaya ya Pangani. Sabas Chambas amewataka wadau wa maeneo yote ya Pangani wasimamie na kutunza miti ya mikoko kuchukua tahadhari kwa kuzingatia athari za kimazingira kupitia wataalam kutoka wakala wa Taifa wa misitu TFS, na Serikali ya Wilaya.

 

Magazeti ya Tanzania leo Machi 7, 2017
Tony Bellew Afikiria Kustaafu Ndondi