Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amesema kuwa Serikali haitawavumilia wawekezaji wenye viwanda wanaokiuka sheria za nchi hasa ya uchafuzi wa mazingira.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya ziara ya uzingatiaji wa sheria ya Mazingira alipotembelea eneo la viwanda mikocheni katika kiwanda cha Iron and Steel Limited, BIDCO limited na Basic elements Limited.

Amesema kuwa amebaini uvunjifu mkubwa wa sheria katika uchafuzi wa mazingira kwenye viwanda hivyo na kiwanda cha Iron Steel na Basic Limited, kila kimoja kimetozwa faini ya sh. Milioni 10 inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili na kutakiwa kufanya marekebisho ya mfumo ya maji.

“Kilichofanyika hapa hakikubaliki na hakiwezekani kufumbiwa macho walichokifanya wamiliki wa kiwanda hiki ni ukiukwaji wa sheria na wamesababisha wananchi wengi waishi katika mazingira hatarishi haiwezekani kuziba mfereji mkubwa kama huu ambao maji taka mengi yalitakiwa kusafiri ikiwemo kutoka viwanda vingine ni hatari sana,”amesema Mpina

Kwa upande wake mratibu wa mazingira kanda ya mashariki kutoka Baraza la taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Jaffar Chimgege amesema kuwa katika kiwanda cha Iron Still Limited imebainika kuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho hawana vifaa vya usalama kazini kitendo ambacho kinatishia afya zao,

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa eneo la Mikocheni ‘B’ wamesema kuwa wana wasiwasi wa afya za familia zao na mazingira kwa ujuma kutokana na sababu kuwa moshi, majitaka na vumbi linatoka katika baadhi ya viwanda hivyo.

 

Kubenea atua Dodoma kuhojiwa
Zari atoa ushauri na faraja kwa wanaosalitiwa