Mahakama nchini Uganda imethibitisha kufunguliwa mashtaka ya uhaini dhidi ya Mpinzani Mkuu wa Rais Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye.

Msemaji wa Mahakama nchini humo, Solomon Muyita aliwaambia waandishi wa habari kuwa sababu kuu ya kumfungulia mashtaka hayo ni kutokana na kuendelea kusisitiza kuwa alishinda katika uchaguzi uliopita na kujiapisha kama Rais wiki iliyopita, siku moja kabla ya Rais Museveni kula kiapo.

Msemaji huyo wa mahakama alisema kuwa Besigye amekuwa akitoa matamko ya ushindi mara kadhaa na kwamba anavitaka vyombo huru kufanya ukaguzi juu ya uchaguzi uliopita.

Besigye alikamatwa muda mfupi baada ya kuonekana kipande cha video kikimuonesha akijiapiza mbele ya mtu aliyevaa mavazi rasmi ya Jaji, wiki iliyopita.

Waziri Mkuu aweka sawa ‘Bunge kurushwa Live’
Jaji Mkuu aipigia mstari Sheria ya Makosa ya Mtandao na uhuru wa kupata taarifa