Rapa anaedaiwa kuongoza kwa kuigwa zaidi kwa mtindo wake wa kurap (flow), Mr Blue ameeleza jinsi alivyopiga teke uvutaji wa dawa za kulevya aina ya bangi na kuhakikisha anakuwa kijana asiyevuta ‘kitu’ zaidi ya hewa.

Blue ambaye hivi sasa ni baba wa familia, ameiambia The Playlist ya 100.5 Times Fm kuwa kuna wakati alijikuta amezama kwenye tabia za uvutaji wa bangi, sigara na unywaji wa pombe kitu ambacho awali hakikuwa sehemu ya tabia zake.

Alisema kuwa anakumbuka baba yake alimwambia kuwa alipokuwa mdogo alikuwa anachukia sana hata moshi wa sigara, hivyo aligundua baadae kuwa alipokuwa amezama wakati ujana na mafanikio ya muziki ‘vimechachamaa’ hapakuwa sehemu yake, ndipo alipoamua kurudi kwenye msitari sahihi.

“Yeah.. hivi sasa nimeacha hivyo vitu. Nimeacha bangi, nimeacha sigara, pombe sinywi,” alisema Mr Blue.

Mkali huyo ambaye video na audio ya wimbo wake mpya wa Mboga Saba aliompa shavu Ali Kiba unafanya vizuri, alieleza kuwa tabia hizo za uvutaji na unywaji vilimuathiri katika masuala yake ya maendeleo lakini alipoachana navyo alijipanga vyema hadi kufanikisha kujenga nyumba tatu.

“Sasa hivi nina nyumba tatu, zote ni muziki… moja naishi, mbili zingine ndio ambazo najaribu kumaliziamalizia… huko Tabata,” Mr. Blue alifungaka.

 

 

UZINDUZI RASIMI WA TAASISI YA MARIDHIANO YA KIDINI WAJA
Video: Makonda awapa wiki mbili Wakuu wa Wilaya kutengeneza Mpango kazi