Mwenyekiti wa TLP, Augustine Lyatonga Mrema ameendelea kung’ang’ania maana halisi ya msemo wa wahenga ‘ahadi ni deni’ hadi atakapohakikisha amelipwa.

Mwanasiasa huyo mkongwe na Mbunge wa zamani wa jimbo la Vunjo amepanga kufika jijini Dar es Salaam wiki ijayo kuifuatilia ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa mwaka jana wakati wa Kampeni alipofika katika jimbo lake. Rais Magufuli aliahidi kumpa kazi baada ya kushinda katika uchaguzi huo.

“Wiki ijayo natarajia kuja Dar, na nafikiri nitaonana na Rais kwanza nimpongeza, halafu nimsisitize anipe nafasi kuna sehemu nazijua tuzisafishe, siwezi kusema mpaka nionane nae ndio nitamueleza,” Mrema amekiambia kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm.

Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya ‘kutumbua majipu’ na kukusanya kodi na kueleza kuwa endapo Rais atapewa ushirikiano watanzania watasherehekea mafanikio yake miaka mitano ijayo.

Zitto Kabwe amvaa Waziri Kitwanga, asema sio saizi yake, ajipima na Rais Magufuli
Kabwe ahoji kulipwa fidia baada ya uchunguzi wa kutumbuliwa jipu