Jeshi la Polisi Mkoani Iringa, linamshikilia Mwasema Rashid (37), aliyekuwa akisafirisha dawa kulevya alizokuwa amezimeza (kete), toka nchini Malawi Kuja nazo hapa nchini.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani  Iringa, Allan Bukumbi amesema siku ya tukio Machi 31, 2023 mtuhumiwa huyo alipofika kijiji cha Mtandika kilichopo Wilayani Kilolo, alianza kujisikia vibaya na kuamua kufika Zahanati na kumueleza Muhudumu wa Afya kuwa anaumwa tumbo.

Kamanda Bukumbi ambaye alikuwa akiongea na Vyombo vya Habari, amesema baada ya mtu huyo kuhojiwa iligundulika kuwa alisafiri kutokea jijini Dar es salaam Machi 17, 2023 kwa kutumia usafiri wa ndege kuelekea nchini Msumbiji na Machi 30, 2023 alirejea kupitia mkoani Mbeya kwa kutumia usafiri wa gari.

“Ilipofika Tarehe 2 Aprili, 2023 hali ilizidi kuwa mbaya ndipo alipoamua kusema ukweli kuwa alimeza pipi za dawa za kulevya aina ya Heroin na hadi sasa ameshatoa pipi 58 kupitia njia ya haja kubwa chini ya uangalizi wa madaktari na Askari Polisi,” amesema Kamanda Bukumbi na kubainisha kuwa upelelezi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.

Serikali yafafanua utekelezaji athari za kiuchumi, kijamii
Makusanyo TRA ni Trilioni 5.9