Mbunge wa Iringa Mjini kupitia tiketi ya (CHADEMA), Peter Msigwa amewapongeza baadhi ya viongozi wa dini akiwepo Askofu Zakaria Kakobe, Askofu Josephat Gwajima, Askofu Benson Bagonza kwa kile walichofanya kukemea baadhi ya matendo ya serikali.
Amesema kuwa hicho kilikuwa kilio chake kikubwa kwa viongozi wa dini kwani Tanzania inapaswa kujengwa na watu wote na si wanasiasa tu.
“Nawapongeza sana baadhi ya viongozi wa dini kama vile Askofu Kakobe, Askofu Gwajima, Askofu Bagonza na Shayo ambao kwa namna moja kimekuwa kilio changu kikubwa pamoja na wananchi wengine kuona viongozi wa dini wanakuwa kimya wakati mambo hayaendi vizuri, Kwa kifupi niwapongeze sana kwa sababu nchi hii inajengwa na sisi sote na mali yetu sote,”amesema Msigwa
Hata hivyo, ameongeza kuwa amesikitiswa na baadhi ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanataka kulifanya Taifa la Tanzania lisiwe la watu wa kufikiri.
- Maalim Seif apanga mkakati mzito
-
Chadema yazidi kupukutika, mwingine aibwaga
-
Lissu afanya muujiza, asimama kwa mara ya kwanza