Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amezindua Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini na Tanzania litakalofanyika nchini kwa wiki moja katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma na Zanzibar,linalokwenda  kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali. 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akizindua Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini na Tanzania Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo, limezinduliwa Novemba 18, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mchengerwa amesema Tamasha la msimu wa utamaduni linajumuisha shughuli mbalimbali za Sanaa na Utamaduni ikiwemo, Maonesho ya harakati zaUkombozi, Sanaa za ufundi za Afrika Kusini na Tanzania, ngoma za asili, maonesho ya yenye historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika.

Baadhi ya wasanii kutoka Afrika Kusini wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini na Tanzania jijini Dar es Salaam.

Amesema, “Hatua hiyo itawapa wageni na watanzania fursa ya kujifunza historia ya mapambano ya kudai uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika na kujionea urithi mkubwa wa historia  uliosalia katika nchi yetu na Tamasha hilo ni jukwaa muhimu la kuonesha na kutangaza bidhaa za kiutamaduni za kiafrika kupitia maonesho ya kazi za mikono za utamaduni na ubunifu, matembezi ya kiutamaduni, muziki wa kiafrika pamoja na ngoma za asili. 

Naibu Waziri wa Utamaduni wa Afrika Kusini, Mcawe Mafu akiongea na umati wa watanzania na Afrika Kusini wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini na Tanzania ambalo linafanyika nchini kuanzia Novemba 18 hadi Desemba 04, 2022 na kusisitiza kuwa nchi hizo mbili ni ndugu wa muda mrefu.

“Tanzania ndio nchi pekee yenye historia ya uhifadhi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, vijana wanapaswa kutambua kuwa Taifa letu lilitoa machozi, jasho na damu kuhakikisha Afrika Kusini na Mataifa mengine ya Afrika yanakua huru na Tamasha hili litaimarisha undugu na kukuza Sekta za Utamaduni na Sanaa ikiwa ni pamoja na kutangaza Utalii, Mila na Desturi.

Watu Bil. 3.5 wanaugua magonjwa ya kinywa
Serikali kuboresha mashamba yake ya Mifugo