Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Kamisheni ya Maafa iweke mipango ya kuzuia maafa siku zote na sio kusubiria maafa yatokee na watakeleze hayo kwa kutumia waatalam mbalimbali.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika ziara yake ya kuwatembelea wananchi waliopata maafa baada ya mvua zinazoendelea kunyesha katika Wilaya tatu za Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwemo maeneo ya Bububu, Kibweni, Kwa Mzushi, Sebleni, Kwa Mtumwa Jeni, Kibonde Mzungu na Ziwa Maboga leo tarehe 14 Novemba 2023.

Amesema Serikali itatekeleza wajibu wake wa kuzuia mafuriko pia amewataka wananchi kupokea maamuzi yatakayoletwa kuhusu mipango ya kuzuia mafuriko nchini na kuwataka wanananchi kutoa ushirikiano wanapoambiwa wahame maeneo yasiyopaswa kujengwa, kuondoa vibali maeneo hatarishi, kupisha ujenzi wa mitaro pamoja na usafi wa mitaro yenyewe.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia alitumia nafasi hiyo kuifariji familia ya Marehemu Aboubakar Abdallah, ambaye ni mkazi wa Sebleni aliyefariki dunia kufuatua mvua hizo za vuli.

Aliyewajibu vibaya Wananchi aondolewe - Dkt. Biteko
Mambosasa agusia ushirikiano kutanzua uhalifu