Wananchi wa Mkoa wa Tabora, wametakiwa kuacha kulitupia lawama Jeshi la Polisi na badala yake wafuatilie Malezi na maadili ya watoto wao, ili kukomesha vitendo vya uhalifu, huku akiwaomba kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha, ili uhalifu na wahalifu waendelee kudhibitiwa.

Wito huo, umetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina msaidizi wa Polisi, Richard Abwao katika mkutano mkuu wa mwaka wa sungusungu, uliofanyika katika Tarafa ya Simbo Wilaya ya Igunga na kuwata kutotumia nguvu wakati wa ukamataji na wahakikishe wanafuata sheria zote.

Amesema, Vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za ukabaji halafu wazazi wao wakaja juu kwa kulakamikia Jeshi la Polisi kutotenda haki ni matokeo ya kutokuwa na maadili mema kwani walikiri kujihusisha na ukataji mapanga na uporaji simu kitendo kilichowashangaza wazazi wao.

Wakati huohuo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polis, Wilbroad Mutafungwa ametoa elimu ya namna ya kuzuia uhalifu na kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi wa kata ya Bukokwa, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani humo.

Mtoto wa Rais ashitakiwa kwa tuhuma za rushwa
Makala: Mtaala Lugha ya Alama ulete ufanisi kwa Kiziwi