Licha ya kupoteza kwa 1-0 kwenye Uwanja wa Manungu Complex katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa Hatua ya Mtoano ‘Play Off’ dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza Tanzania Prisons, rasmi Klabu ya Mtibwa Sugar imesalia Ligi Kuu Tanzani Bara.

Mtibwa Sugar imesalimika katika hatua hiyo, kufuatia ushindi wa 3-1 iliyouvumna katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza Hatua ya Mtoano ‘Play Off’ uliopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Jumapili (Julai 03).

Bao pekee la Tanzania Prisons katika mchezo wa leo Jumatano (Julai 06) limepachikwa wavuni kwa ufundi mkubwa na Mshambuliaji Mudathir Abdallah, ambalo halikutosha kuharibu mipango ya Mtibwa Sugar iliyoibuka na ushindi wa jumla wa 3-2.

Kwa mantiki hiyo Tanzania Prisons inaendelea na mpango wa kusaka nafasi ya kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kucheza mchezo mwingine wa Mtoano ‘Play Off’ dhidi ya JKT Tanzania inayotokea Ligi Daraja la Kwanza.

Mchezo wa Mkondo wa Kwanza kwa Miamba hiyo utachezwa Jumamosi (Julai 09), Uwanja wa Jenerali Isamuyo jijini Dar es salaam, kabla ya kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili Jumatano (Julai 13) katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mshindi wa jumla katika mchezo huo atapanda Daraja na kucheza Ligi Kuu Msimu wa 2022/23 ambao utaanza rasmi Agust 13.

Kiswahili chaundiwa mikakati kuiteka Dunia
Bosi mpya TPA akutana na agizo la siku saba