Mwalimu mmoja  aliwapa wanafunzi  kazi waandike kitu ambacho kila mtu angetamani kuwa, insha ya mwanafunzi mmoja ilisomeka hivi.

Natamani kuwa smart phone kwani wazazi wangu wanapenda sana smart phone kuliko wanavyonipenda mimi, hawana muda na mama, wanajali sana smart phone zao kuliko wanavyonijali mimi mpaka wamesahau kunihudumia, pindi wanapokuwa wanafanya kazi zao za msingi za ofisini hata mlio mmoja wa smartphone ukiita hupokea simu hizo haraka lakini sio mimi hata nikilia hakuna anayeshughulika na mimi, pindi babangu anapotoka kazini anakuwa na muda na smart phone yake na sio muda na mimi, babangu na mamangu hupenda kucheza game kwenye smart phone zao lakini sio kucheza na mimi alimazia hivyo.

Ni jambo la kujifunza hasa kwa hawa wazazi wa kidigitali ambao muda wao mwingi wanaupelekea kwenye mitandao ya kijamii na kusahau familia zao, hii story fupi inaonesha ni jinsi gani mtoto anatamani muda na mzazi lakini anaukosa kwa kuhisi mama au baba hana mapenzi naye, anapenda simu yake kuliko anavyompenda yeye, ndio maana watoto wanafanyiwa vitendo vya ajabu, lakini hawasemi kwasababu mama au baba hajajenga mazoea ya kukaa na kuzungumza na watoto wao.

Wakati ndio huu wa kubadilika mama baba kuwa na muda na wanao, zungumza nae umjue vizuri mwanao.

 

 

Majaliwa awasimamisha kazi Maofisa Misitu wanne, Asimamisha uvunaji magogo Rufiji
Griezmann: Bado Ninamuhitaji Diego Simeone