Mlipuko wa mtungi wa hewa ya sumu aina ya Chlorine uliotokea katika bandari ya Aqaba nchini Jordan, umesababisha vifo vya watu 13 na wengine zaidi ya 250 kujeruhiwa.
Mlipuko huo, umetokea baada ya mtungi wa hewa ya sumu uliokuwa na uzito wa tani 25 kudondoka na kulipuka, wakati ukipakiwa katika roli kutoka kwenye meli iliyokuwa imebeba shehena ya mizigo.
Katika taarifa yake, Serikali ya Jordan imeeleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Waziri Mkuu wa Jordan, Bisher Al- Khasawneh ametembelea eneo ulipotokea mlipuko huo, kwa lengo la kujionea madhara yaliyotokea.