Mhamasishaji na mratibu wa maandamano ya kupinga mkataba wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Serikali ya Tanzania, Deus Soka hajatokea kwenye maandamano yaliyopangwa kuanzia Wilayani Temeke na kuishia Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kutaka kushiriki maandamano hayo ambayo yalipigwa marufuku mwishoni mwa wiki, ambayo yalipangwa kufanyika hii leo Juni 19, 2023.

Maandamano hayo yalipigwa marufuku na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam huku likisema taarifa yake iliyofikishwa Polisi, muhusika alijibiwa kuwa hayataruhusiwa na Polisi iliimarisha ulinzi maeneo mbalimbali ya katikati mwa Jiji la Dar es Salaam.

Deus Soka ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, na aliyewahi kugombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, Juni 15 alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba huo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro alisema hayatakuwepo na muhusika ameshajibiwa.

Young Africans yakita kambi Ivory Coast
Simba SC kumng'oa STOPPER wa Cameroon