Makamu Mwenyekiti wa Young Africans Fredrick Mwakalebela anaamini matokeo ya sare kadhaa waliyoyapata msimu huu, yamewanyima nafasi ya kutimiza lengo la kuwa Mabingwa wa Tanzania Bara.

Mwakalebela ametoa kauli hiyo, ikiwa tayari Simba SC wameshatazwa kuwa Mabingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo, huku jana wakitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC na kufikisha alama 80.

Mwakelebela amesema kama isingekua matokeo ya sare yaliyowakabili wakati wa utawala wa Kocha kutoka nchini Burundi Cedic Kaze, basi leo mashabiki na wanachama wa Young Africans wangekua na kicheko cha ubingwa.

“Tulipata droo nyingi hapo awali ndio zilitupotezea mwelekeo wa malengo yetu, lakini kwa sasa tumepata kocha mzuri, kwa hiyo watakaofanikiwa kwenda Kigoma waje kifua mbele ikiwezekana wakiwa wamevaa suti.”amesema Mwakelebela

Ushindi wa jana Alhamis (Julai 15) dhidi ya Ihefu FC, umeifanya Young Africans kufikisha alama 73 zinazoioweka katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku ikisaliwa na mchezo mmoja mkononi.

Mkakati wa 'KOPA MBUZI LIPA MBUZI' kuanza, chanjo za mifugo zatakiwa vijijini
Tozo mpya za miamala, Mwigulu atia neno