Jeshi la Polisi Mkoani Geita limesema, Mwalimu Emmanuel Chacha (35), wa Shule ya msingi Igaka, iliyopo Kata ya Isulabutundwe, Tarafa ya Kasamwa Wilayani Geita, amefariki baada ya kuchomwa kisu na mwalimu mwenzake.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amesema tukio hilo lilitokea Machi 15, 2023 majira ya saa tatu asubuhi, baada ya Mwalimu huyo kuchomwa na kisu kwenye eneo la chembe ya moyo.

Uhalifu: Polisi yanasa Bastola, wahalifu wakimbia

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo.

Amesema, “mtuhumiwa naye ni Mwalimu, mwanaume (35), jina linahifadhiwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Igaka kilichopo Kata ya Isulwabutundwe, Tarafa ya Kasamwa.

Kmanda Jongo amesema, “uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na mtuhumiwa amekamatwa, amehojiwa na amekiri kufanya tukio hilo.” na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombea uongozi wa kitengo cha Elimu ya kujitegemea.

Ataja njia aliyotumia kupata kazi baada ya miaka mitano
Msuva, Samatta kuungana na wenzao Misri