Baada ya kocha Hans van der Pluijm kuandika barua ya kujizulu, kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi atakiongoza kikosi cha klabu hiyo kongwe hadi kocha mkuu mpya atakapoanza kazi.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema George Lwandamina raia wa Zambia ataanza kazi rasmi Novemba Mosi.

Tayari Lwandamina yuko jijini Dar es Salaam.

Awali ilielezwa kwamba Pluijm atakuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga kabla ya mwenyewe kuamua kujiuzulu.

Ligi Ya PL Yaingiza Wanane Tuzo Ya Mchezaji Bora Duniani
Video: Tanzania na Morocco zatiliana saini mikataba 22